.

.

Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) imepokea Shilingi bilioni 57 za kununua Bidhaa za Afya

 eliaonesmo@gmail.com

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

Bohari ya Dawa Tanzania (MSD)  imepokea Shilingi bilioni 57 ikiwa ni fedha za robo mwaka ya kwanza kati Shilingi bilioni 200 zilizotengwa kwa kununua bidhaa za Afya kwa mwaka mzima.



Haya yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Bwana Mavere Ali Tukai katika mkutano wake na vyombo vya Habari wakatia akitoa taarifa ya Utekelezaji na Maboresho ya Mnyororo wa Ugavi wa bidhaa za Afya uliofanyika Jijini Dodoma.


"Katika awamu ya sita,fedha kwaajili ya ununuzi wa bidhaa za Afya zimetolewa kwa kiwango kikubwa kupita nyakati zote. Mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 134.9. Kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 hadi kufikia mwezo huu Oktoba 2022 MSD imeshapokea fedha zote ya robo ya mwaka ya kwanza ambayo ni Shilingi bilioni 57 kati ya silingi bilioni 200 zilizotengwa kwa kununua bidhaa za Afya kwa mwaka mzima".


Aidha Bwana Tukai amesema MSD imeendelea kusambaza bidha za Afya katika vituo vya Afya 7,153 katika kanda zake 10 zilizowekwa kimkakati.


"MSD imendelea na zoezi la usambazaji wa bidhaa za Afya kwenye vituo vyote vya afya vya Serikali ambavyo ni 7,153 kupitia kanda zake 10 zilizowekwa kimkakati. Vituo hivi vya kutolea huduma za Afya vipo kuanzia ngazi ya Zahanati vituo vya Afya na Hospital vituo vyote hivi vinahudumiwa na kanda zetu 10nilizotangulia kuzitaja kwenye utangulizi. MSD pia ina maduka ya jamii sita yaliyopo Mpanda (katavi),Mount Meru(Arusha),Ruangwa (Lindi),Mbeya, Chato(Geita) na Muhimbili (Dar er salaam) ambayo yanasaidia kusogeza huduma kwa wananchi

Usambazaji wa bidhaa za Afya hufanyika mara 6  kwa mwaka ambapo kila kituo hutakiwa kupelekewa bidhaa za Afya kila baada ya miezi miwili kwa mujibu wa kalenda ya usambazaji".


Pia MSD imejikita katika miradi mbalimbali ya Viwanda  inayozalisha vifaa tiba na vifaa kinga kama vile Barakoa,Mipira ya Mikono,Rangi mbili,Vimiminika na Dawa za ngozi.


"Kiwanda cha uzalishaji wa Barakoa ni mradi wa kwanza kutekelezwa MSD katika nyanja ya uzalishaji. Mradi huu ulianza kutekelezwa mwezi Agost 2020 baada ya kusimikwa kwa mtambo wa kisasa wa kuzalisha barakoa kwaajili ya matumizi ya watumishi katika sekta ya Afya kama kifaa kinga (PPE) pamoja na watumiaji wengine kama nyenzo ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya maradhi ya mfumo wa njia ya hewa hasa Uviko 19 kiwanda kimefanikiwa kupunguza gharama ya bei za Barakoa na pia kuhakikisha vituo vya Umma vya kutolea huduma vinakua na nyakati zote"


"Viwanda vya bidhaa za Afya IDOFI,viwanda hivi vipo katika kijiji cha Idofi Makambako mkoani Njombe ,miradi hii ipo kwenye hatua mbalimbali ikihusisha viwanda vya Mipira ya Mikono,Vidonge,Rangi mbili,Vimiminika na Dawa za ngzi, ujenzi huu unaendelea na katika mpango mkakati wake MSD imedhamilia kukamilisha viwanda hivi ili viweze kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za Afya ".



Naye Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye ni Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amegusia kuhusu Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ambalo lilikuwa ni moja ya swali la Mwandishi, amesema kuwa nia Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata matibabu ya aina yeyote na kwa gharama yetote na kuondokana na adha wanayokutana nayo wananchi wanapokosa fedha kwaajili ya matibabu.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments: