Mwandishi wetu,Arusha
Wakati wakazi wawili wa wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara,Yusuph Athuman(40) na Faisal Abdi (41) wakihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya uhujumu uchumi baada kukutwa wakiuza Kakakuona ambaye ni nyara za serikali dereva wao hukumu yake kusomwa Novemba 30 mwaka huu.
Wakazi hao wa Simanjiro kabla ya kufungwa, walikamatwa na askari wa Mamlaka ya usimamizi wanyamapori kanda ya kaskazini na polisi Arusha baada ya kuweka mtego.
Watuhumiwa hao, walikamatwa katika katika hoteli ya Koridor Spring jirani na hoteli ya ya Kibo Palace jijini Arusha, wakiwa na kakakuona huyo wakiuza bila kuwa na kibali na bila kujua wanaotaka kuwauzia ni maafisa wa TAWA.
Kamanda wa TAWA kanda ya kaskazini, Kamishna msaidizi mwandamizi, Peter Mbanjoko alisema baada ya kukamatwa walifikishwa polisi ambapo walikiri kufanya biashara hiyo na kesi yao iliandaliwa na juzi kufikishwa mahakamani.
"baada ya kukiri makosa na upelelezi wake kukamilika walifikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria"alisema
Watuhumiwa wote walipandishwa mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi namba 8/2022 mbele ya Hakimu Mkazi Arusha,Fadhili Mbelwa.
Wakili wa Serikali Tarsila Asenga akishirikiana na Janeth Sekule , Penina Mollel na Mwendesha wa TAWA Getrude William Kariongi waliwasomea mashitaka watuhumiwa hao na kukiri makosa.
Akisoma uamuzi baada ya washitakiwa hawa kusomewa mashitaka yao na kukiri, Hakimu Mbelwa aliwatia hatiani na kuwahukumu kifungo cha miaka 20, Yusuph Athman na Faisal Abdi.
Mtuhumiwa Mtuhumiwa mmoja ambaye ni dereva wa gari hilo,Alfani Lugazo alikana mashitaka hukumu yake itakuwa Novemba 30 kwaajili ya utetezi.
0 comments:
Chapisha Maoni