.

.

SHIRIKA LA CORDS LATOA MSAADA WA MAHINDI TANI 7.1 KWA KAYA 395 WILAYANI LONGIDO

NA MWANDISHI WETU: LONGIDO.



Shirika la Utafiti, Maendeleo na Huduma kwa jamii( CORDS) jana limekabidhi  tani 7.1 za mahindi kwa kaya 395 za vijiji viwili  vya wilaya ya Longido mkoa wa Arusha ili kukabiliana na uhaba wa chakula.

Akizungumza wakati wa ugawaji mahindi hayo, ,Afisa idara ya miradi ya shirika la CORDS ,Martha Katau alisema wameamua kutoa mahindi ya msaada baada ya kubaini kaya nyingi zinakabiliwa na njaa.



"tumekuwa na miradi kadhaa hapa Longido, ikiwepo ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, lakini tumebaini kuna upungufu wa chakula kwa kaya nyingi na hivyo tumeona tusaidie walau kidogo"alisema



Alisema katika mgao huo, kijiji cha  Ildonyo kaya 165 zimepatiwa tani 2.6 na kijiji cha Orpurkel Kaya 230 zimepatiwa tani 4.5 ili kusaidia kukabiliana na upungufu wa chakula.

Kaimu Afisa kilimo wa wilaya ya Longido, Mariam Fivawo  alisema  ukame umesabisha uhaba wa chakula katika maeneo mengi ya wilaya hiyo ambayo asilimia 95 ya wananchi ni wafugaji.

Hata hivyo, aliwataka wananchi wenye mifugo kujitahidi kuuza baadhi ya mifugo yao  ili waweze kununua chakula cha bei nafuu ambacho tayari kimepelekwa na serikali katika wilaya hiyo.



Mmoja wa wanufaika wa msaada huo, Witness Alais  alisema msaada huo wa mahindi utasaidia sana kukabiliana na njaa kwani licha ya kukosa chakula lakini pia hata maziwa ya mifugo hawana kutokana na mifugo mingi kufa kwa ukame na iliyobaki haiwezi kuzalisha maziwa kwa wingi.

"tunashukuru shirika la CORDS kwa kutupa msaada huu ambao  utasaidia hasa akina mama na watoto ambao wanashida kubwa zaidi ya chakula"alisema

Shirika hilo pia wiki iliyopita lilitoa msaada wa mahindi  tani 12  kwa kaya 553 katika  vijiji vya Idonyonaado  na Emuruwa  katika kata ya Mfereji wilaya ya Monduli  mkoa Arusha.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni