.

.

TFS,CYCA KILIMANJARO KUHAMASISHA UPANDAJI MITI KATIKA MAENEO YA UKANDA WA MLIMA KILIMANJARO

 KILIMANJARO-

NA SALMA SEFU.

Kwa kutambu umuhimu wa siku ya Muungano  Taasisi zinazozunguka Mlima Kilimanjaro ikiwemo Shamba la miti la West Kilimanjro,Shirika la hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na wadau mbali mbali wameadhimisha siku hii kwa kupanda miti na kutoa elimu ya Umuhimu wa utunzaji mazingira na maliasili  jumuishi katika maeneo ya ukanda wa Mlima Kilimanjaro.



Tukio hilo la upandaji miti limefanyika December 9 katika eneo la Shamba la Miti la west Kilimanjaro lililopo Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro likifuatiwa na ziara ya kutembelea maeneo ya shamba hilo ambapo imeelezwa kuwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Aidha Bw.Masawanga yahaya ambaye ni  Mhifadhi Mkuu shamba la miti la west Kilimanjaro  amesema lengo la tukio hilo ni kuonyesha umuhimu wa Mlima Kilimanjaro na Bionowai zinazozunguka mlima huo na umuhimu wa Bionowai katika maisha ya binadamu lakini pia kutangaza Nchi yetu ya Tanzania ili kuweza kuendelea kuwa namba moja  katika Afrika.



Tumekutana hapa kuuambia ulimwengu na Watanzania kwa ujumla kwamba tuna tunu ambayo sehemu nyingine hawana hivyo tunatakiwa kuitunza na kuilinda,kumekuwa na matukio ya moto Mlima Kilimanjaro kwa kutunza maeneo yanayozunguka mlima itaasaidia kuepukana na majanga ya moto na athari nyingine pia,tunaamini tukitunza mazingira yanayozunguka mlima na mlima pia utakuwa salama.,Bw.Masawanga yahaya 

West kilimanjaro imepanda Miche laki nne  kwa kipindi cha mwaka mmoja huku Miche ipatayo elfu 20 ikitolewa kwenye taasisi mbali mbali na wananchi kwaajili ya kupandwa  ikiwa ni jitihada za kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira.



Baadhi ya wadau walioshiriki katika zoezi hilo pia hawakusita kuzungumza.

Bw. Mensieur Elly ambaye ni Mratibu wa shirika la vijana la connecting youth connecting Afrika Tanzania lenye mlengo wa kuwaunganisha vijana kwenye nyanja tofauti tofauti ikiwemo kutunza mazingira,kufanya uhifadhi na kuhamasisha masuala ya mabadiliko ya tabia ya Nchi amesema kwa kutambua uwepo wa changamoto ikiwemo njaa na mabadiliko ya tabia ya Nchi shirika hilo linawajumuisha vijana ndani na njee ya Tanzania kuwa na sauti moja na kuhamasisha uhifadhi jumuishi na mabadiliko ya tabia ya Nchi.



Tunaungana na mamlaka za hifadhi za misitu kwa maana ya wakala wa huduma za misitu ambao wapo kwenye Ecolojia na wana vivutio vingi vya utalii,kwa kampeni hii ya leo tutakuwa tunaungana kila mwaka kwa kushirikiana na vijana wengine nje na ndani ya nchi kuungana pamoja kuja kwenye maeneo ya hifadhi ya mlima kilimanjaro kuhamasisha uhifadhi jumuishi na mabadiliko ya tabia ya Nchi  kwa kuanzia kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi kuweza kupata elimu,kutembelea maeneo yote yenye vivutio vya utalii,na kupanda mlima.Bw. Mensieur Elly

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni