.

.

MKUU WA WILAYA YA ARUMERU AELEKEZA MIRADI YA BOOST KUKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA UBORA

Na Onesmo Elia Mbise -Arusha 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela Kaganda aelekeza miradi ya uboreshaji miundombinu katika shule za Msingi kukamilika kwa Wakati na kwa ubora uliokusudiwa.

Mhe.Kaganda amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya BOOST katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo Serikali imetoa milioni 961.5 za uboreshaji miundombinu ya elimu kwenye Shule za Msingi.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela Kaganda akishiriki ujenzi wa msingi wa shule ya msingi ya mkondo mmoja Kikatiti katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo Serikali imetoa Milioni 961.5 fedha za mradi wa BOOST kwaajili ujenzi wa miundombinu ya Shule za Msingi katika Halmashauri hiyo Picha na Mpiga picha wetu.

Aidha, Mhe. Kaganda amesema Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imejipanga vyema kuendelea kuwaletea wananchi wake maendeleo ambapo imetoa fedha nyingi za maendeleo katika sekta ya elimu,afya, na maji.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela Kaganda akishiriki ujenzi wa msingi wa shule ya msingi ya mkondo mmoja Kikatiti katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo Serikali imetoa Milioni 961.5 fedha za mradi wa BOOST kwaajili ujenzi wa miundombinu ya Shule za Msingi katika Halmashauri hiyo Picha na Mpiga picha wetu.

Mhe.Kaganda amewataka wataalum wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kuwa na ubora uliokusudiwa kwani anmza ya Serikali ni kuwawezesha Watoto wa kitanzania kupata Elimu bora katika mazingira rafiki.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni