.

.

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTLII AITAJA TAWIRI KUWA TAASISI YA KIMKAKATI

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Hassan Abbas ameitaja Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania ( TAWIRI ) kuwa ya kimkakati na umuhimu mkubwa katika sekta ya Maliasili na utalii ambapo tafiti za TAWIRI ni dira katika kuimarisha uhifadhi na kukuza utalii nchini.

Akizungumza na wajumbe wa timu ya menejimenti wakati wa ziara katika taasisi hiyo , Dkt. Abbas amesema kipaumbele cha Wizara ya Maliasili na Utalii ni kuendelea kuhifadhi maliasili iliyopo kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Aidha, Dkt. Abbas ameeleza TAWIRI ni daraja muhimu kwa ustawi wa taasisi nyingine za uhifadhi kwa kutoa ushauri wa kitaalum kuhusiana na wanyamapori " sekta ya uhifadhi inaitegemea TAWIRI kutoa mbinu bora zitakazo wezesha uhifadhi na ustawi wa wanyamapori na makazi yao"ameeleza Dkt.Abbas

Dkt. Abbas ametoa wito kwa Viongozi wa TAWIRI kuhakikisha umma unapata matokeo ya Tafiti za wanyamapori zinazofanyika ili kuzitumia kwa maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dkt. Ernest Mjingo amemshukuru Katibu Mkuu kwa ziara na nakuahidi kupokea maelekezo yote kwa ajili ya utekelezaji.



Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni