Polisi ya Nigeria imetangaza kwamba, kwa akali watu 50 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya watu wanaobeba silaha kuishambulia jamii ya watu wa Gidan Aku ilioko katika eneo la Wukari katika jimbo la Taraba nchini humo. Garba Umar Gavana wa Jimbo la Taraba amewataka wakaazi wa eneo hilo kushirikiana na serikali na vyombo vya usalama katika kuwatia nguvuni wahusika wa shambulio hilo. Wakati huohuo Msemaji wa Polisi ya Nigeria imeeleza kuwa, kwa akali watu 17 wameuawa baada ya kushambuliwa na wabeba silaha katika kijiji kimoja kilichoko katika jimbo la Taraba. Taarifa zinasema kuwa, watu hao walifanya unyama mwingine wa kuteketeza kwa moto nyumba za kijiji hicho na kuwaacha makumi ya wanakijiji hao bila ya makazi. Polisi imeeleza kuwa, wachungaji mifugo wa jimbo la Taraba ndio waliosababisha shambulio hilo.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 comments:
Chapisha Maoni