Wakati dunia ikijiandaa na wiki ya kimataifa ya chanjo ambayo hufanyika kila mwaka katika wiki ya mwisho ya mwezi wa April, Shirika la afya ulimwenguni WHO limetoa wito likitaka kuchukuliwa hatua zaidi ili kuhakikisha watoto na watu wengine wa kawaida wanapatiwa njanjo dhidi ya magonjwa hatarishi. George Njogopa na ripoti kamili.
(Taarifa ya George)
WHO inasema kuwa utoaji kinga umeweza kuepusha zaidi ya vifo vya watu milioni 2-3 kila mwaka duniani kote ambao walikuwa hatarini na magonjwa kama kupooza, kuhara, tetenasi.
Kwa maana nyingine WHO imesema kuwa suala la njanjo linaendelea kupewa kipaumbele na limeingizwa katika mpango maalumu wa kimataifa unaojulikanma " Program ya upanuz i wa njanjo mradi ambao baaaye mwaka huu utaadhimisha mwaka wake wa 40.
Shirika hilo limesema kuwa licha kwamba kumekuwa na juhudi mbalimbali za kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki chanjo, lakini hadi sasa bao kunasafari ndefu ya kufikia shabaha iliyowekwa.
Hata hivyo limesema kuwa litaendelea kufanya kazi na wahisani wake ikiwemo kubuni mbinu mpya ya utoaji njanjo kupitia teknolojia za kisasa kama vile internet.
0 comments:
Chapisha Maoni