Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amesema kuwa, uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya bara la Afrika umesababisha kuibuka migogoro, mapigano na uporaji wa maliasili na utajiri wa bara hilo. Akizungumza kwenye mkutano wa tatu wa usalama wa Afrika uliofanyika nchini Ethiopia, Rais al Bashir amesema kuwa, nchi hizo za Magharibi zimekuwa na nafasi kubwa katika kuzusha mifarakano, mapigano na migogoro katika bara la Afrika, hali inayowasababishia matatizo makubwa watu wa bara hilo. Rais wa Sudan amesema kuwa, usalama katika bara la Afrika bado ni tete pamoja na kuwepo juhudi za kieneo na kimataifa za kuimarisha usalama barani humo. Rais al Bashir amesisitiza kuwa, kuna ulazima kwa viongozi wote wa Kiafrika kufanya juhudi za kurejesha amani na utulivu barani humo. Rais Omar al Bashir amewataka wakuu wa nchi za Kiafrika kustafidi na maliasili na suhula zilizopo kwa lengo la kulistawisha bara hilo na kutatua matatizo yaliyopo kwa njia za amani, matatizo ambayo yalisababishwa na madola ya Magharibi.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 comments:
Chapisha Maoni