.

.

Jeshi la Kenya: Tutaendelea kuwasakama al Shabab

Jeshi la Kenya: Tutaendelea kuwasakama al Shabab
Jeshi la Kenya limetangaza kuwa, litaendeleza operesheni zake za kijeshi dhidi ya wanachama wa kundi la kigaidi nakitakfiri la ash-Shabab.

Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na jeshi hilo imesema kuwa, operesheni zilizopewa jina la 'Linda Boni' kwa ajili ya kuondoa hatari tarajiwa ya kundi hilo la kigaidi la ash-Shabab dhidi ya mji wa Lamu, na ambazo zilianza wiki moja iliyopita, zimekuwa na mafanikio makubwa. Imeongeza kuwa, jeshi la Kenya limefanikiwa kukusanya ripoti muhimu za wanachama hao wa kigaidi sanjari na kuongeza doria katika maeneo yote ya mpakani ya nchi hiyo na Somalia.

 Hii ni katika hali ambayo kundi la ash-Shabab tawi la al-Qaidah nchini Somalia limekuwa likifanya hujuma na mashambulio kadhaa nchini Kenya sanjari na kuwalenga maafisa usalama wa nchi hiyo
.
 Hivi kariburi pia wanachama wa genge hilo walitoa vitisho dhidi ya serikali ya Nairobi wakitishia kufanya shambulio jipya nchini humo
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni