.

.

Mkutano wa nchi za East Africa waendelea Bujumbura

Mkutano wa nchi za East Africa waendelea Bujumbura

Kikao cha ushirikiano na ustawi wa kijamii wa nchi za ukanda wa eneo la Mashariki mwa Afrika, kinaendelea jijini Bujumbura, Burundi licha ya mgogoro wa kisiasa kuendelea kushuhudiwa nchini.

Kikao hicho ambacho ni cha nne kati ya makongamano ya viongozi wa nchi za eneo la Mashariki mwa Afrika, kilianza jana Jumanne mjini Bujumbura. Katika ufunguzi wa kikao hicho, Joseph Butore Makamu wa Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo alisema kuwa, kufanyika kikao hicho kwa kuhudhuriwa na viongozi wa kieneo, ni kwa lengo la kuanzisha ushirikiano wa pamoja katika masuala ya kisiasa kieneo.

 Butore aliongeza kuwa, kueneza ustawi wa kijamii na kiuchumi kupitia njia ya ushirikiano wa serikali kuu, ni miongoni mwa malengo makuu ya kikao hicho cha siku mbili. Amesema kuwa, ni suala lisilo na shaka kwamba, kuimarishwa ushirikiano wa nchi za eneo kunaweza kuboresha juhudi za kukabiliana na umasikini na kuboresha maisha ya raia wa nchi hizo za Mashariki mwa Afrika. Nchi za Mashariki mwa Afrika, zinajumuisha Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda, Tanzania, Eritrea, Ethiopia, Djibouti, visiwa vya Ushelisheli, Comoro, Somalia, Sudani Kusini na Mauritius
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni