Mtekaji nyara awaachia huru abiria na kuwazuia wengine
Maafisa wa Misri wamefahamisha kwamba mtu aliyedhaniwa kujihami kwa miripuko aliiteka nyara ndege ya shirika la ndege la Misri iliyokuwa ikitokea Alexandria kwenda Cairo mji mkuu wa nchi hiyo hii leo na kumlazimisha rubani wa ndege hiyo kutuwa katika kisiwa cha Cyprus
.
Shirika la ndege hiyo EgyptAir limesema kwamba baada ya ndege hiyo aina ya Airbus 320 kutuwa katika uwanja wa ndege wa Larnaca huko Cyprus mtekaji nyara huyo aliwaachia huru watu wote waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo isipokuwa abiria wanne raia wakigeni pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo.Rais wa Cyprus Nicos Anastasiade punde baada ya tukio hilo alikuwa na haya ya kueleza.
Kiasi watu 60 ikiwemo wahudumu saba walikuwemo ndani ya ndege hiyo kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na maafisa wa Misri na Cyprus.Shirika la habari la Cyprus limeripoti kwamba mtekaji nyara huyo huenda nia yake inashusiana na masuala ya kibinafsi na kwamba mtalaka wake yupo nchini Cyprus.
0 comments:
Chapisha Maoni