.

.

Bw. Ban Ki-Moon azitaka pande zote za Syria zisimamishe vita huko Aleppo


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon ametoa taarifa kupitia msemaji wake akifuatilia kudorora kwa hali ya usalama mjini Aleppo nchini Syria, na kuzitaka pande zote za Syria zisimamishe vita mara moja na kuepuka kuwadhuru raia.
Taarifa pia imetoa mwito kwa Marekani na Russia kuongeze juhudi, na kusaidia pande zote za Syria kusimamishe vita, ili kupunguza maumivu kwa raia, na kusukuma mbele mchakato wa mazungumzo ya amani ya Geneva.
Wakati huohuo, waziri wa Mambo ya nje wa Russia Bw. Lavrov jana alijadiliana na mwenzake wa Marekani Bw. Kerry kwa njia ya simu kuhusu hali ya Syria na pande hizo mbili zilizitaka pande zinazopambana nchini Syria zifuate utaratibu wa kusimamisha vita.
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni