.

.

Mamilioni ya wanawake duniani waandamana kupinga Urais wa Donald Trump




Rais Donld Trump aliapishwa Ijumaa hii kwa sherehe mjini Washington DC, lakini hiyo haimaanishi kuwa mambo yametulia – ndio yameanza.
Jumamosi hii, mamilioni ya wanawake duniani, waliandamana kupinga kuapishwa kwake kama rais wa 45 wa Marekani. Maandamano makubwa zaidi yalikuwa Marekani hususan kwenye mji mkuu, Washington.
Wanawake hao walioungwa mkono na mastaa kibao pamoja na wanaume walioependa kuwaunga mkono, walikuwa na ujumbe mmoja tu, kuwa hawatakuwa kimya kwa miaka minne yote ya uongozi wa Trump.
Kulikuwa na maandamano kwenye zaidi ya miji 600 duniani kote huku waandamaji wakiwa na mabango mengi yanayomdhihaki na kumlaani Trump.
Mastaa walioshiriki kwenye maandamano hayo ni pamoja na Katy Perry, Madonna, Scarlett Johansson, Jake Gyllenhaal, Emma Watson, Ashley Judd, Cher, America Ferrera, Kristen Stewart, Charlize Theron, Whoopi Goldberg, Cynthia Nixon, Charlotte Church, Yoko Ono, Helen Mirren, Julia Roberts, John Legend, Amy Schumer na wengine.
Takriban watu milioni 2.2 wanaaminika kuwa waliandamana kutetea haki zao na za binadamu.
Pamoja na miji mingi ya Marekani, miji mingine duniani iliyokuwa na maandamano makubwa ni pamoja na London, Paris, Berlin, Edinburgh, Rome, Prague, Amsterdam, Stockholm, Athens, Copenhagen, New Delhi, Brussels, Mexico City, Barcelona, Manila, Toronto, Madrid, Geneva, Cardiff na Sydney.
Hizi ni picha zaidi:

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

1 comments
Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni