LONGIDO
Mesoni Kashiro (15) mkazi wa kijiji cha Gelailumbwa kata ya Gelailumbwa wilaya Longido Mkoani Arusha, ameshambuliwa na mume wake Namendea Lesiria kwa kushirikiana na rafiki yake ambaye jina halijafahamika kwa kosa la kumwaga dawa ya mfugo aina ya mbuzi.
Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani humo Atunagile Chisunga amesema kuwa watuhumiwa wapo kituo cha polisi Longido, na kesho wanatarajia kufikishwa mahakamani, lakini mama huyo yupo kituo cha afya Longido kwa matibabau zaidi.
"Huu ni ukatili kabisa kwanza ameolewa akiwa na umri mdogo, wamempiga wakiwa wamemfunga kamba na kumtundika kwenye miti" amesema Chisunga.
0 comments:
Chapisha Maoni