Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejiment na utawala Bora Deogratius Dejembi ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kuzifanyia kazi taarifa za CAG.
Naibu Waziri Dejembi ameyasema hayo wakati wa mahafali ya mafunzo ya awali ya uchunguzi yaliyofanyika kwa muda wa miezi mitano kuanzia April Hadi Septemba katika chuo cha polisi CCP kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
Amesema kuwa TAKUKURU inatakiwa kuzifanyia kazi taarifa hizo ili kukomboa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema TAKUKURU ni chombo nyeti Cha uchunguzi hivyo kinatakiwa kupambana na rushwa kwa kufuatilia taarifa zote za CAG ili thamani ya pesa iweze kuonekana.
Aidha amewataka kuwa mabalozi wema wa TAKUKURU katika vituo walivyopangiwa kwa kuwa ni wajibu wao Kufuata taratibu na muongozo ili kulinda maadili.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Salum Hamduni amesema kuwa serikali imeelekeza fedha nyingi kwenye kutekeleza majukumu kwa wananchi lakini kumekuwa na vitendo vya ubadhirifu wa Mali ya uma vinavyofanywa na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wasio waaminifu.
0 comments:
Chapisha Maoni