Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameitaka Mamlaka inayoshughulika na utoaji wa vitambulisho vya Taifa NIDA iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi kuongeza kasi ya uzalishaji wa vitambulisho vya Utaifa ili kumsaidia mwananchi kupata wepesi wa kutambulika anapokuwa na mahitaji mbalimbali.
Waziri Mkuu Mjaliwa ametoa kauli hiyo katika Kongamano la sita la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi leo Jijini Dodoma ambapo ameitaka Mamlaka hiyo kuongeza kasi ya utoaji wa vitambulisho vya Taifu huku pia akizitaka Taasisi za kifedha kuendelea kutoa mikopo kwa riba nafuu.
"Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi ambako mnatoa Vitambulisho vya Taifa, Mamlaka hii ya Vitambulisho vya Taifa NIDA iongeze kasi ya utoaji wa vitambulisho ili kuwawezesha Wananchi kutambulika wanapohitaji huduma mbalimbali zinazohitaji Vitambulisho".
Sambamba na hayo Waziri mkuu ameitaka mikoa ambayo haijaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi waanzishe kwa mwaka huu wa fedha 2022-2023.
"Sasa ni wakati muhimu wa kuanzisha vituo vya uwezeshaji katika mwaka wa Fedha 2022/2023 na inatakiwa suala hili litekelezwe kwa jitihada zote".
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda,biashara na uwekezaji Dkt Ashantu Kijaju amesema bado kuna changamoto ya watanzania kushindwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kiwango cha kimataifa.
"Bidhaa zetu zinakwenda kwenye masoko lakini bado tuna tatizo la kujua ubora unaohitaji kule duniani".
Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara Stanbic Bank Bi Kai Mollel aliyemwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu ambao pia ndio wadhamini wakuu wa Kongamano hili la uwezeshaji wananchi kiuchumi amesema mbali na utoaji wa huduma za kifedha pia wamejikita katika kuwawesha Wanachi kuweza kufaidika na fursa zinazotokana na uwekezaji kama kauli mbiu inavyoakisi.
"Sisi kama Bank tunafanya huduma za kifedha kwa wafanyabiashara na Taasisi za Umma lakini pia tumejikita katika kuwawezesha Wananchi na Watanzania kuweza kufaidika na fursa zinazotokana na uwekezaji".
Kongamano la Sita la Uwezeshaji wananchi kiuchumi limebebwa na kauli mbiu isemayo ''uwezeshaji wananchi katika uwekezaji''
0 comments:
Chapisha Maoni