Na Jackline Lendava-Dodoma.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, amewataka vijana kujitambua ,kuwa na uthubutu pamoja na kujiwekea malengo .
Amesema huwezi kupewa lifti kama umekaa nyumbani wakati una safari ya kwenda Daresalam lazima usogee Barabarani ukisimama tu wanajua wewe ni msafiri utapewa lifti .
Hayo yamejiri jijini Dodoma Katika Wilaya ya Chamwino wakati wa Kongamano la Vijana la fursa zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maendeleo ya Vijana.
Katambi Amesema Lengo la Kongamano hili ni kumwezesha kijana kujitambua na atambue nafasi yake kwenye Jamii,
“kila kijana anatakiwa kupambana kivyake lakini akumbuke Serikali yetu ni Moja”
Aidha Naibu Waziri Katambi amewasisitiza Vijana kufanya kazi kwa bidii na kuacha tabia ya kuwa Tegemezi kwa Wazazi wao,
Ameongeza kuwa Vijana wengi wanafikra ya utegemezi na hawataki kufanya kazi hawataki kujituma, Amesema Kama mnavyofahamu, vijana duniani kote ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza na kujenga uchumi wa mataifa yao.
"Ili tuwe na Taifa lenye Nguvu tunahitaji Vijana wachapakazi wanao jituma hata vitabu vya Dini vimewataka Vijana kufanya kazi” Alisema Mhe. Katambi
Kwa upande wake Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora. Amewasisitiza Vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali Amesema Serikali hii ya hawamu ya sita imejipanga kutokomeza dibwi la Vijana wasio na kazi za kufanya, wasio na Ajira.
"Ajira inaweza ikawa kwenye kilimo inaweza kuwa kwenye mifugo au kwenye Boda Boda na mama lishe, ndiyo maana tumekutana hapa kwa lengo la kujengana kupitia haya mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya amewapongeza Vijana kwa kuwa na mwitikio Mkubwa wamejitokeza zaidi ya Vijana mia Tatu ambao watapatiwa mafunzo mbalimbali namna ya kupambana na fursa tunataka Vijana wajiajili wenyewe.
0 comments:
Chapisha Maoni