.

.

SERIKALI IMEKUSANYA SH. BILIONI 852.9

 Na Jackile Lendava-Dodoma.

SERIKALI imesema katika mwaka wa fedha 2021/22 imekusanya sh.bilioni 852.9 sawa na asilimia 109.5 ya lengo ambapo lengo lilikuwa kukusanya sh.Bilioni 779.03 sawa na asilimia 33.5.

Hayo yamelezwa hii leo Oct. 26,2022 Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa uwekezaji Ofisi ya Msajili wa Hazina Lightness Mauki wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa Ofisi hiyo katika mwaka huu wa fedha.



Amesema mapato hayo yamekusanywa kutoka katika mapato yasiyo na kodi ambayo yanajumuisha gawio, michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi na mapato mengineyo.

Kadhalika amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imeendelea na juhudi za kusimamia utendaji wa kampuni ambazo Serikali inaumiliki wa hisa chache ikiwa ni pamoja na kufanya majadiliano na wabia wenza na kusimamia kwa ukaribu matumizi yasiyo ya lazima ambapo ongezeko la gawio kwa wanahisa limeonekana.

Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imeanzishwa kupitia sheria ya msajili wa Hazina (mamlaka na majukumu) sura 370 lengo kuu la kuanzishwa kwa OMH ni kusimamia uwekezaji na Mali zingine za Serikali katika Taasisi na mashirika ya umma, pamoja na kampuni ambazo Serikali inaumiliki wa hisa au kuna maslahi ya umma kwa niaba ya Rais na kwaajili ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni