NA JACKLINE LENDAVA.
DODOMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia watumishi wote walioondolewa kazini kwa kugushi vyeti warudishiwe michango yao waliyokatwa kwenye mishahara yao.
Hayo yameelezwa hii leo oct. 26 2022 na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana na wenye ulemavu Prof. Joyce Ndalichako alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa michango watakayorudishiwa ni 5% waliyokuwa wakichangia katika mfuko wa jamii na NSFF.
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameridhia kuwa watumishi wote waliiondolewa kazini kwa kugushi vyeti warudishiwe michango yao tu waliyokatwa kwenye mishahara ya watumishi na kuwasilishwa kwenye miguko ya hifadhi ya jamii ambayo ni 5% PSSSF na 10% kwa ASSF waliyokuwa wakichangia na si ambayo mwajiri alikuwa akichangia" Prof. Ndalichako
Aidha Prof. Ndalichako amesema kuwa mwajiri atatakiwa kujaza hati ya ridhaa kwa aliyekuwa mwajiri wake na mwajiri kuwasilisha kwenye mifuko pamoja na nyaraka nyingine kwa kuzingatia taratibu na miongozo kwa mifuko husika.
"Marejesho ya michango ya watumishi hao yataanza kufanyika kuanzia 01 Novemba, 2022 hivyo mtumishi husika atatakiwa kuwa na picha za passport size mbili, nakala ya taarifa za kibenki ya akaunti iliyo hai na nakala ya kitambulisho cha Taifa au mpiga kura au leseni ya udereva" Prof. Ndalichako
Agizo hilo limetokana na shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani 01 Mei 2022 kuomba wafanyakazi walipwe mafao kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
0 comments:
Chapisha Maoni