NA JACKLINE LENDAVA.
DODOMA.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) imeagizwa kuzuia vitendo vyovyote vya Rushwa nchini vitakavyojitokeza wakati wa zoezi la kurudishiwa michango kwa walioachishwa kazi kwa kugushi vyeti.
Wito huo umetolewa Oktoba 26, 2022 na waziri wa nchi, ofisi ya Rais, menejiment ya umma na utawala bora mh. Jenista Mhagama kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu la watumishi wote waliotolewa kazini kutokana na kugushi vyeti.
"Nawaagiza TAKUKURU kwanzia sasa wahakikishe wanatumia kila mbinu mkakati kuzuia vitendo vyovyote vya Rushwa katika kukamilisha zoezi hili, eneo lingine niwasihi watumishi wote wawe waaminifu" Mh. Jenista mhagama
Aidha mh. Mhagama ameagiza kila ofisi kuwa na dawati la msaada ili kutoa maelekezo ya jinsi ya ujazwaji wa fomu ya kurejeshewa michango yao na watumishi wote kuwa waaminifu.
"Ili kuhakikisha zoezi hili linaenda kwa ufanisi naagiza ofisi zote za serikali wahakikishe wanaandaa madawati ya misaada ili kuwasaidia namna ya kujaza mikataba hiyo, hatutarajii wahusika hao wakifika ofisini hawajui wamuone nani, madawati yote yatoe maelekezo kwa urahisi" mh. Jenista Mhagama.
Kwa upande mwingine mh. Mhagama amesema kuwa wamefikia mfumo wa uoanishwaji na uainishwaji kwa mwajiriwa kuwa na Jina kamili, check namba, alama za vidole pamoja na namba ya nida.
" Kama serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan jambo hili halijitokezi tena na halijirudii kwa hiyo tunaendelea kuweka mifumo wa kuhakikisha kwamba vyeti vya taaluma vinahakikiwa"
Serikali iliendesha zoezi maalumu la uhakiki wa vyeti kwa kushirikiana na baraza la mtihani la Taifa (NACTE) kuanzia Oct. 2016-April, 2017 na watumishi 14,516 waliondolewa kazini.
0 comments:
Chapisha Maoni