.

.

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII KWA WATUMISHI WA UMMA WAWEKEZA KATIKA MIRADI YA VIWANDA

 Na Jackline Lendava-Dodoma.

Katika kuunga mkono sera ya serikali ya kukuza uchumi kupitia maendeleo ya viwanda, mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF) umewekeza katika miradi minne ya viwanda ambayo ni ranchi ya mifugo na machinjio ya kisasa ya Nguru Hills Morogoro, kiwanda cha kusindika chai Mponde, kiwanda cha bidhaa cha ngozi Kilimanjaro na kiwanda cha kuchakata tangawizi Same.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa PSSSF CPA Hosea Kashimba Novemba 09, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa mfuko kupitia idara ya manunuzi umeendelea kufanya manunuzi wa mujibu wa aheria ya mwaka 2021 na ulipata matokeo kwa asilimia 94.



"Kwa upande wa ulipaji wa mafao mfuko umelipa mafao mbalimbali yanayotolewa kwa mujibu wansheria ambapo jumla ya trilion 6.32 kwa pensheni ya uzeeni, pensheni iliyoahirishwa, fao la ulemavu, fao warithi, fao la upotevu wa ajira, fao la ugonjwa na mkopo wa nyumba" CPA Hosea.

Mkurugenzi Hosea amesema kuwa katika kuhakikisha kwamba kunakuwepo na huduma bora katika ofisi zote za PSSSF kumekuwepo na dawati la malalamiko, PSSSF kiganjani kwa ajili ya wananchi kujihudumia wenyewe kwa simu na uhakika wa wastaafu kwa kutumia alama za vidole.



Aidha CPA Hosea ameeleza malengo yao ya baadae kuwa ni kuongeza vituo vya uhakika katika halmashauri mbalimbali na kuanzisha utaratibu wa kujihakiki kqa simu janja, kila taarifa ya wanachama iwe kwenye mfuko na usimamizi bora wa miradi ili kupata matarajio kusudiwa.

" Matarajio mengine ya mfuko ni kutumia mifuko ya tehama, asilimia 85 ikiwa malengo ni kutumia kwa asilimia 100 ifikapo 2023, katika shughuli za mfuko hivyo kuboresha utoaji huduma kwa wananchi, kurahisisha uandikishaji wanachama na uletaji wa madai kupitia mtandao na kuhakikisha mifumo ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa umma inasomana na mifumo mingine kutoka taasisi nyingine za umma ya watoa huduma" CPA Hosea. 



CPA Hosea amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo anayapa kipaumbele na msukumo wa hali ya juu maswala yahusuyo hifadhi ya jamii kwa ujumla.

" Wakati wa kuunganisha mifuko PSSSF ilirithi madeni ya serikali yaliyohakikiwa yenye thamani ya bilioni 731.40 mpaka sasa kiasi cha bilioni 500 kimelipwa na serikali" CPA Hosea.

Ameendelea kwa kusema kuwa "nirudie kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutambua deni la michango kabla ya 1999 maarufu kama per 99 liability ambalo ni trilioni 4.60 kwa kutoa hati fungani maalum yenye thamani ya trilioni 2.17" 

Kwa kipindi cha miaka minne mfululizo mfuko wa PSSSF umekaguliwa na kupata hati safi na kuwa mashindi wa tuzo inayotolewa na NBAA kwa utunzaji bora wa mahesabu ya mwaka 2019/20 katika sekta ya hifadhi ya jamii na bima.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni