.

.

WAHANDISI 33,773 WAMESAJILIWA NCHINI TANZANIA

 Na Jackline Lendava-Dodoma.

Imeelezwa kuwa bodi ya usajili wa wahandisi tangu kuanzishwa kwake imesajili wahandisi 33,773 na wahandisi 26,000 wapo sokoni.



Hayo yameelezwa na msajili wa bodi ya wahandisi (ERB) mhandisi Bernard Kavishe wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza utekelezaji wa majukumu ya bodi ya wahandisi (ERB) na vipaumbele kwa mwaka wa fedha 2022/23.

"Tangu bodi imeundwa mwaka 1968 imesajili wahandisi wa ngazi mbalimbali 33,773 tumeshasajili makampuni ya kiushauri 398 ambapo katika hayo 275 ni ya kitanzania na 123 ni ya nje, tumeshasajili maabara 40, tumeshasajili wahandisi independent consulting 30 pia tumeanza kusajili wahandisi sanifu 1979" Mhandisi Bernard 



Mhandisi Bernard ameeleza vipaumbele vya mwaka 2022/23 kuwa ni kuhuisha leseni za wahandisi wataalamu ambazo zinaisha muda wake wa matumizi Desemba 31, 2022, kufanya marekebisha ya sheria ya usajili wa wahandisi na kutoa elimu kuhusu masuala ya usalama, afya na mazingira katika kutekeleza shughuli mbalimbali za kihandisi hapa nchini.

"Nikianza na hii ya kuhuisha leseni zoezi hili litaanza kutekelezwa Novemba 28, 2022 vipaumbele vingine ni kujenga uwezo wa wataalamu wa ndani wa kada ya uhandisi nchini kwa kuratibu na kiendesha mafunzo endelevu ya ujuzi mbalimbali katika kutekeleza shughuli za kihandisi hapa nchini, kuhimiza nidhamu na maadili kwa wataalamu wa kada ya uhandisi katika kutekeleza majukumu na kuratibu na kutoa ithibati ya mitaala ya fani ya uhandisi inayotolewa na vyuo mbalimbali kwa kushirikiana na tume ya vyuo vikuu" Mhandisi Bernard.



Aidha Mhandisi Bernard ameongeza kuwa katika miradi ya kimkakati kwa upande wao ni darasa kubwa kwa kuwa huja na teknolojia mpya akitolea mfano gari moja ambayo hutoka kwenye mafuta ya dizel mpaka kuendeshwa kwa mfumo wa umeme  hivyo wahandisi wa ndani ya nchi kuzidi kuongeza ujuzi.

"Swala la rushwa ni swala la kitaifa na ndo maana Tanzania inapambana nayo, sisi tukitambua kama kuna dalili za rushwa sisi tunawakabidhi kwa TAKUKURU ambao ndo wahusika wa jambo hilo lakini sisi tunapambana nao pia niombe wananchi endapo ukaona kuna dalili za rushwa toa taarifa kwa TAKUKURU, wananchi waache tabia ya kuwahifadhi watu wanaofanya hivo" Mhandisi Bernard 



Majukumu ya bodi ya wahandisi ni kuratibu na kusimamia kikamilifu mienendo na shughuli za kihandisi nchini kwa kugawanyika katika kusajili wahandisi na kampuni za ushauri wa kihandisi, kuendeleza wahandisi kitaaluma, kuhakikisha kuwa kazi za kihandisi zinafanywa na wahandisi zinafanywa na wahandisi waliosajiliwa na kampuni za ushauri wa kihandisi zilizosajiliwa na kutoa idhibati ya vyuo na mitaa ya uhandisi kwa kushirikiana na kamisheni ya vyuo vikuu nchini

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments: