.

.

SERIKALI KUTEKELEZA MIRADI 12 YA KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI TANZANIA.

 Na Jackline Lendava-Dodoma.

Serikali imetenga bilioni 111.8 kwa ajili ya kutekeleza miradi 12 ya kampuni ya Huduma za Meli Tanzania (MSCL) kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Ndg.Eric Hamissi wakati akizungumza na waandishi wa habari hii leo Novemba 1,2022 Jijini Dodoma na kuelezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha wa 2022-2023.

"Katika miradi hiyo 12 kuna miradi 4 ambayo ni mipya, miradi 5 ni ya ukarabati ambapo MV Mwanza ni miongoni ambayo serikali imetenga bilioni 24 na MT Sangara. Miradi 3 inaendelea kutekelezwa tangu mwaka wa fedha uliopita." Ndg. Erick.



Aidha kati ya bilioni 111.8 za utekelezaji wa miradi hiyo bilioni 59 zimetengwa kwa ajili ya Ziwa Victoria ambapo kati ya hizo bilioni 24 zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa MV Mwanza Hapa kazi Tu na mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 73.

Pia Mkurugenzi huyo amesema wanaendelea na ukarabati wa MV Umoja ambapo imetengewa Bilioni 1.7, MV Ukerewe imetengewa bilioni 3.5 na ukarabati wa Meli ya Mafuta ya MT Nyangumi yenye uwezo wa kubeba lita 350 nayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 6.8.

"Tutajenga Meli nyingine Mpya kabisa ya Mizigo ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 3000 ambapo katika mwaka huu imetengewa bilioni 12 na hii itasaidia sana kuunganisha nchi yetu na Uganda yenye soko kubwa sana la bidhaa ambayo inahitaji zaidi ya tani elfu sita hivyo kukamilika kwa meli hii itasaidia nchi kuingiza mapato makubwa," Mkurugenzi Eric

Mkurugenzi Eric amesema kuwa kati ya Bilioni 111.8 Ziwa Tanganyika imetengewa kiasi cha Shilingi bilioni 53.9 itakayotumika kwa ajili ya kutekeleza miradi Mipya na kukarabati meli zinginine ikiwemo Meli Kongwe yenye miaka 105 ya MV Liemba.

"Katika Ziwa Tanganyika kuna mradi mpya wa ujenzi wa Meli Mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo ambapo kwa mwaka huu wa fedha imetengewa jumla ya Bilioni 12 na mradi mwingine mpya kwa upande wa Ziwa Tanganyika ni ujenzi wa Cherezo ambao nao umetengewa bilioni 12 na itamalizika ndani ya miezi 14, bilioni 12 pia imetengwa kwa ajili ya meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo itakayokamilika ndani ya miezi 24." Mkurugenzi Eric.



Kampuni hiyo kabla ya changamoto ya kutetereka ilikuwa inaajiri vijana zaidi ya 300 na baada ya changamoto hiyo kuisha kampuni imeajiri wafanyakazi 120 huku miradi yote ikikamilika itaongeza idadi ya ajira na mapato yataongezeka kwa taifa.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni