.

.

WAUGUZI NA WAKUNGA TUMIENI LUGHA NZURI

Na WAF - Shinyanga.

Wauguzi na wakunga waaswa kuwa na lugha nzuri na ubunifu wa hali ya juu katika kuwahudumia wagonjwa  Hospitalini.



Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga  Bi. Ziada Sellah katika kikao na wawakilishi wa wauguzi na wakunga kutoka katika wilaya za Msalala, Ushetu na Kahama Mkoani Shinyanga kujadili changamoto mbalimbali katika kada hiyo.

“Fanyeni kazi ya uuguzi na ukunga kwa moyo wote, kumekuwa hakuna kauli nzuri kwa wagonjwa na ndugu za wagonjwa wetu wetu pindi wanapokuja katika Hospitali zetu” amesema Bi. Ziada.

"Wauguzi na wakunga wenzangu tubadilike, lugha kwa wagonjwa ikiwa nzuri kila mtu ata tamani kuja kutibiwa katika hospitali zetu " Amesema Bi. Sellah



Ameendelea kusema Wauguzi na Wakunga wanahitaji kuwapa faraja wagonjwa na wateja wetu ili kuboresha huduma katika vituo vyao.

"Twendeni tukaboreshe huduma kwa kadri tulivyo fundishwa kwa kufuata kanuni taratibu na miongozo ya Wizara ya Afya ikiwa ni kuwapa faraja wagonjwa wetu " Amesema Bi. Sellah 

Aidha Bi. Sellah amewasihi wauguzi na wakunga kuwa wabunifu katika kuwahudumia wagonjwa

"Unapokuwa mbunifu kwenye kumhudumia mgonjwa itasaidia kuongeza utoaji wa huduma bora katika vituo vyetu na kuwavutia wagonjwa wengi kuja Hospitalini" Amesema Bi. Sellah

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni