NA ONESMO ELIA MBISE-ARUSHA.
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kujiajiri wao wenyewe katika sekta ya habari na utangazaji kwa kanzisha vyombo mbalimbali vya mtandaoni kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia ili kuharakisha zoezi la kuipasha jamii habari kwa wepesi na haraka zaidi.
Mkurugenzi wa shirika la MAIPAC Bw Musa Juma akitoa hotuba.PICHA na Marystela Bryson. |
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali nchini MAIPAC ambae pia ni mjumbe wa MISA TANZANIA Bw Musa Juma wakati akihutubia wahitimu na wazazi katika mahafali ya 16 ya ChuoCcha Uandishi wa Habari na Uangazaji Fanikiwa yaliyofanyika katika ukumbi wa PPS jijini Arusha.
Bw Musa ambae alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo amesema kuwa ulimwengu wa sasa umekuwa, haswa katika eneo la sayansi na teknolojia hvyo wana habari wanapaswa kukimbia na ukuaji huo kwa kuanzisha vyombo vya habari vya mitandaoni ambavyo vitawasaidia wao kujiajiri kitaaluma.
Wahitimu Wa Chuo Cha Uandishi wa Habari na Utangazazji Fanikiwa Ausha. PICHA na Marystela Bryson |
Mbali na hayo amewataka wahitimu hao wa ngazi ya Stashahada kuzingatia maadili wawapo kazini lakini pia kuwa wabunifu katika kuandika habar za mazingira,kilimo,uchumi, na hata mabadiliko ya hali ya hewa ili kusaidia kuwaweka katika mazingira mazuri zaidi ya kihabari.
Nae mkuu wa chuo hicho Bwana Andrea Ngobole, amewataka wazazi wa wahitimu hao kuwaendeleza zaidi vijana hao katika chuo kikuu ili waendelee kupata elimu zaidi juu ya tasnia ya habari na sekta nyinginezo.
Mkuu wa Chuo cha andishi wa habari na Utangazaji Fanikiwa Bw Andrea Ngobole akitoa hotuba kwa wahitimu.PICHA NA Marystela Bryson. |
Aidha katika Mahafali Hayo wahitimu wapatao 40 wamehitimu mafunzo yao ya umahiri katika Tasnia ya habari na utangazaji ambapo pia wamedhamiria kwenda kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya habari na utangazaji.
katika picha ni wahitimu wa Chuo Cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Fanikiwa arusha. |
Pamoja sana hii safi
JibuFuta