.

.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ARIDHISHWA NA MIKAKATI YA KUBORESHA SEKTA YA MIFUGO MONDULI

Mwandishi wetu -ARUSHA.

Serikali yaeleza kuridhishwa na mikakati ya wilaya ya Monduli,mkoa Arusha kuboresha sekta ya Mifugo kutokana na ujenzi wa miundombinu na kuboresha Minada

Naibu Waziri wa maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega ametoka pongezi hizo Leo February 20,2023 wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Naalarami na viongozi wa Serikali wilayani Monduli.



 Waziri Ulega amesema miundombinu ambayo imeendelea kuboreshwa na wilaya ya Monduli itasaidia sana kukuwa kwa sekta ya Mifugo.

Naibu Waziri Ulega amewataka wafugaji katika wilaya hiyo kuanza kufuga kisasa ikiwepo kutenga maeneo ya nyanda za malisho ili kukabiliana na Ukame.

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Fred Lowassa Akizungumza katika ziara hiyo,amemshukuru Naibu Waziri wa Mifugo, Ulega kutembelea jimbo la Monduli kukagua miundombinu ya mifugo .



Lowassa amesema Wananchi wa Kata ya NAALARAMI wamefarijika sana kwa ugeni huu na wametuma salamu za Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia sekta ya Mifugo.

Amesema katika wilaya hiyo ,ambayo ni ya wafugaji wanamkakati wa kuwasaidia wafugaji kielimu Ili iwe rahisi kuboresha maisha ya badala ya kuwasisitiza wauze mifugo.

"Hawa ndugu zangu kazi ambayo wanajua ni ufugaji pekee hawajuwi biashara nyingine zaidi ya mifugo Sasa mikakati yetu ni kusomesha vijana wengi zaidi Ili kuleta mabadiliko katika jamii kwa kuamini vijana watakuja na ujuzi tofauti"amesema

Lowassa amesema Rais Samia amesikia kilimo Chao Cha maji , barabara na soko la akina mama wa mji wa mto wa mtu wa mbu.



"Tunashukuru sana Rais Samia amekubali maombi yangu na barabara kilomita 20 kutoka Kigongoni hadi Engaruka inajengwa lakini pia analeta mradi wa maji na anajenga soko la wanawake Mtowambu "amesema

Mkuu wa wilaya ya Monduli Selemani Mwenda amesema wilaya hiyo imejipanga vyema kutatua kero za Wananchi wa Monduli na kuna Mahusiano mazuri baina ya Mbunge na watendaji wa Serikali.

Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni