Waziri Dr.Jafo azindua kitabu Cha maarifa ya asili katika utunzwaji wa Mazingira kilichoandaliwa na MAIPAC
Mwandishi wetu,Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dr. Seleman Jafo amezindua kitabu Cha kwanza Cha aina yake Cha maarifa ya asili katika uhifadhi wa Mazingira ,misitu na Vyanzo maji.
Kitabu hicho kimeandaliwa na taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) Kwa kushirikiana na taasisi ya CILAO kimetokana na simulizi za wazee la Mila ya kimasai, wanawake na vijana wa jamii hizo katika wilaya za Ngorongoro, Longido na Monduli.
Waziri Dr. Jafo amepongeza MAIPAC Kwa kuja na mradi huo wa aina yake na kueleza serikali itawaunga mkono.
"Huu ni mradi wa kwanza wa aina yake nawapongeza MAIPAC Kwa kazi nzuri kwani pia nimeona documentary nzuri na Nina Imani UNDP na wafadhili wengine wataendelea kuwapa fedha zaidi kuendeleza mradi huu"amesema
Amesema uhifadhi wa mazingira kwa maarifa ya asili ni muhimu kwani , maarifa hayo yalikuwa yanatumika toka enzi za mababu ambapo imesaidia kutunza misitu, vyanzo vya maji na mazingira na kitabu hicho kitakuwa njia sahihi ya kueneza elimu ya utunzaji wa Mazingira kwa njia ya asili.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa MAIPAC Mussa Juma amesema kuwa kitabu hicho kimeelezea simulizi za jamii ya masai wanavyotumia taratibu na mila zao katika kutunza mazingira, vyanzo vya maji na misitu ambapo Mradi huu ulizinduliwa rasmi Agosti 27,2022 jijini Arusha na Mkuu wa mkoa wa Arusha, ambaye aliwakilishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa Arusha.
Amesema Mradi huo umefadhiliwa na programu ya miradi midogo ya mfuko wa mazingira Duniani(GEF) unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) nchini Tanzania chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais –Idara ya Mazingira.
Afisa maendeleo ya jamii mkoa Arusha Bi. Blandina Nkini ameipongeza MAIPAC kwa kuwa shirika pekee lililokuja na mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa kutumia maarifa ya asili na kuwa moja ya shirika la mfano mkoani Arusha kati ya mashirika 1114 yaliyosajiliwa mkoani Arusha na kuwaomba wafadhili wengine kuwasaidia katika kutekeleza miradi yao.
Mratibu wa miradi midogo UNDP kupitia shirika la mfumo wa Mazingira duniani (GEF) Faustine Ninga ameipongeza MAIPAC kwa kukamilisha kuchapa vitabu na kuandaa video na machapisho ya mradi huo.
"nawapongeza kwa kutoa kitabu cha utunzaji wa mazingira kwa maarifa ya asili na tutaendelea kushirikiana katika miradi mingine ya mazingira wanayotarajia kuitangaza hivi karibuni."amesema
Katibu wa baraza la mila la kimasai Tanzania Amani Lukumayi ameipongeza MAIPAC kwa kuandaa kitabu cha aina yake kinachoelezea umuhimu wa maarifa ya asili katika uhifadi wa mazingira, utunzaji wa vyanzo vya maji na misitu kwani utakuwa urithi muhimu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Katika uzinduzi huo pia waliohudhuria viongozi kutoka halmashauri za wilaya ya Monduli, Longido na Ngorongoro na kuelezea mikakati Yao kuendelea kuhifadhi na kutunza Mazingira.
Pia viongozi wa Serikali mkoa Arusha,Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na viongozi wa vijiji na mashirika yasiyo ya kiserikali walishiriki .
0 comments:
Chapisha Maoni