.

.

SERIKALI YAENDELEZA JITIHADA ZA KUREJESHA MBWA MWITU HIFADHI YA TAIFA SERENGETI

 Uhifadhi wa Ikolojia.

Na Onesmo Elia Mbise

Serikali kupitia Taasisi zake TAWIRI na TANAPA imeendelea  na zoezi endelevu la kuwarejesha mbwa mwitu ndani  ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwa ni kuhakikisha mbwa mwitu wanaendelea kuhifadhiwa katika mfumo _ikolojia_  ya Serengeti.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuwapokea mbwa mwitu wapatao 20  waliozaliwa Hifadhi ya Taifa Mkomazi na kuletwa Hifadhi ya Taifa Serengeti kabla ya kuachiwa huru, Dkt. Emmanuel Masenga ambaye ni Mtafiti Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti Serengeti amesema kuwa matokeo ya tafiti yanaonyesha kuwa sababu kuu za kutoweka kwa mbwa mwitu katika hifadhi ya Serengeti ni magonjwa (Rabies and Canine Distemper Virus) na ongezeko la idadi ya simba na fisi pamoja na kuuwawa na wananchi wanapotoka nje ya hifadhi.

Aidha, Dkt. Masenga  amesema jitihada za Serikali  za kuwarejesha mbwa mwitu ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ni zoezi endelevu na lilianza tangu mwaka 2011 kwa lengo la kuhifadhi mbwa mwitu kwa ajili ya kutunza bioanuwai na kuendeleza utalii.

Dkt. Masenga  amesema kama inavyofahamika jukumu kubwa la Taasisi  ya  Utafiti  Wanyamapori  Tanzania (TAWIRI) ni kufanya  tafiti  za wanyamapori, hivyo TAWIRI  inaendelea kufanya tafiti za kina za kuhakikisha kuwa mbwa mwitu wanaendelea kuhifadhiwa katika mfumo ikolojia wa Serengeti.



Share on Google Plus

About Dira Ya Maisha

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Chapisha Maoni